Job 38

Sehemu Ya Nne: Mungu Anazungumza

(Ayubu 38–41)

Bwana Anamjibu Ayubu

1 aKisha Bwana akamjibu Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli. Akasema:
2 b“Nani huyu atiaye mashauri yangu giza
kwa maneno yasiyo na maarifa?

3 cJikaze kama mwanaume;
nitakuuliza swali,
nawe unijibu.


4 d“Ulikuwa wapi nilipoweka misingi ya dunia?
Niambie, kama unafahamu.

5 eNi nani aliyeweka alama vipimo vyake?
Hakika wewe unajua!
Ni nani aliyenyoosha kamba ya kupimia juu yake?

6 fJe, misingi yake iliwekwa juu ya nini,
au ni nani aliyeweka jiwe la pembeni,

7 gwakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja,
na malaika wote walipokuwa wakipiga kelele kwa furaha?


8 h“Ni nani aliyeifungia bahari milango
ilipopasuka kutoka tumbo,

9 inilipoyafanya mawingu kuwa vazi lake,
na kuyafungia katika giza nene,

10 jnilipoamuru mipaka yake,
na kuiweka milango yake na makomeo mahali pake,

11 kniliposema, ‘Unaweza kufika mpaka hapa wala si zaidi;
hapa ndipo mawimbi yako yenye kiburi yatakapokomea’?


12 l“Umepata kuiamrisha asubuhi ipambazuke,
au kuyaonyesha mapambazuko mahali pake,

13 yapate kushika miisho ya dunia,
na kuwakung’uta waovu waliomo?

14 mDunia hubadilika kama udongo wa mfinyanzi chini ya lakiri;
sura yake hukaa kama ile ya vazi.

15 nWaovu huzuiliwa nuru yao,
nao mkono wao ulioinuliwa huvunjwa.


16 o“Je, umepata kufika kwenye chemchemi za bahari?
Au kutembea mahali pa ndani pa vilindi?

17 pUmewahi kuonyeshwa malango ya mauti?
Umewahi kuiona milango ya uvuli wa mauti?

18 qJe, wewe unafahamu ukubwa wa dunia?
Niambie kama unajua haya yote.


19 r“Njia ya kufika kwenye makao ya nuru ni ipi?
Nako maskani mwa giza ni wapi?

20 sJe, unaweza kuvirudisha kwenye makao yake?
Unajua njia za kufika maskani mwake?

21 tHakika unajua, kwa kuwa ulikuwa umeshazaliwa!
Kwani umeishi miaka mingi!


22 u“Je, umeshawahi kuingia katika ghala za theluji,
au kuona ghala za mvua ya mawe,

23 vambazo nimeziweka akiba kwa ajili ya wakati wa taabu,
na kwa ajili ya wakati wa vita na mapigano?

24 wNi ipi njia iendayo mahali umeme wa radi unapotawanyiwa,
au mahali upepo wa mashariki unaposambaziwa juu ya dunia?

25 xNi nani aliyepasua mifereji kwa ajili ya maji mengi ya mvua yaendayo kasi
na njia ya umeme wa radi,

26 yili kusababisha mvua kunyeshea mahali pasipokaliwa na mtu,
jangwa lisilo na yeyote ndani yake,

27 zili kuitosheleza nchi ya ukiwa na jangwa,
na majani yaanze kumea ndani yake?

28 aaJe, mvua ina baba?
Ni nani baba azaaye matone ya umande?

29 abBarafu inatoka tumbo la nani?
Ni nani azaaye ukungu kutoka mbinguni,

30 acwakati maji yawapo magumu kama jiwe,
wakati uso wa vilindi vya maji unapoganda?


31 ad“Je, waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia?
Waweza kulegeza kamba za Orioni?

32 aeWaweza kuyaongoza makundi ya nyota kwa majira yake,
au kuongoza Dubu na watoto wake?

33 afJe, unajua sheria zinazotawala mbingu?
Waweza kuweka utawala wa Mungu duniani?


34 ag“Waweza kuiinua sauti yako mpaka mawinguni,
na kujifunika mwenyewe na gharika ya maji?

35 ahJe, wewe hutuma umeme wa radi kwenye njia zake?
Je, hutoa taarifa kwako kukuambia, ‘Sisi tuko hapa’?

36 aiNi nani aliyeujalia moyo hekima
au kuzipa akili ufahamu?

37 ajNani mwenye hekima ya kuyahesabu mawingu?
Ni nani awezaye kuinamisha magudulia ya mbinguni

38 akwakati mavumbi yawapo magumu,
na mabonge ya udongo kushikamana pamoja?


39 al“Je, utamwindia simba jike mawindo,
na kuwashibisha simba wenye njaa

40 amwakati wao wamejikunyata mapangoni mwao,
au wakivizia kichakani?

41 anNi nani ampaye kunguru chakula
wakati makinda yake yanamlilia Mungu,
yakizungukazunguka kwa ajili ya kukosa chakula?

Copyright information for SwhKC